Wednesday, May 25, 2011

RYAN GIGGS KUICHAKACHUA NDOA YAKE...?!


RYAN GIGGS
Pamekuwa na minong'ono kwamba mchezaji wa Man United ya Uingereza,Ryan Joseph Giggs ametembea na mmoja wa aliyekuwa mshiriki katika kipindi cha televisheni cha Big Brother,Imogen Thomas
IMOGEN THOMAS
Tuhuma hizo za muda mrefu na kabla ilipitishwa sheria mahsusi kuwalinda watu maarufu kutotolewa hadharani mambo yao ya siri kwa sababu wanazozifahamu wao wenyewe.Lakini ghafla bin vuu, mbunge kwa tiketi ya chama cha Liberal,John Hemming,akiwa bungeni akateleza ulimi na kumtaja mchezaji huyo anayelindwa na sheria hiyo kuwa ni Ryan Giggs wa Man United, na amekuwa mmoja wa wanaharakati ambaye amekuwa akipinga kwa mchezaji huyu kulindwa na sheria hiyo. Huku wakati huo huo watumiaji wa mtandao wa Twitter ambao walikuwa wameshalinyaka jina hilo na kuanza kumegeana ndogo ndogo kwa sasa Giggs yuko kwenye wakati mgumu sana hasa ndoa yake na kwa sasa habari hiyo imeshaenea duniani kote...!
 

No comments:

Post a Comment