Friday, May 20, 2011

WEMA SEPETU MCHARUKO WAMPANDA AMSUTA CHAZ BABA


Chaz baba akipata mafundo ya mate toka kwa wema enzi za uhai wa penzi lao
      Mrembo alietumia nafasi ya sanaa vibaya Wema sepetu amefunguka dhidi ya tuhuma zilizotapakaa kila kona ya nchi kuwa karudiana na Chaz baba na kuwa hamtaki tena Diamond kwakua hayawezi mabo ya kitandani.

                 Wema alisema kuwa bado anampenda sana Diamond na hana hisia zozote za kuachana na kijana huyo msharobalo alietingwa na mawazo ya kuachwa muda wowote kwani ndege usipomshika vizuri hukuachia manyoya ndiyo hali aliyonayo diamond kwa sasa.
                 "Chaz baba nilishamwaga na nilishamwambia kuwa siwezi kuwa nawe tena ila anatumia magazeti kuandika habari za uongo kwani mimi ndiye niliempa umashuhuri mpaka akawa anaandikwa mara kwa mara sasa ameona haandikwi kama zamani ndiyo maana ameamua kutafuta ujiko kupitia mimi" wema alitonya haya kwa kimombo.
                  Inasemekana Chaz baba amekuwa akimsumbua wema katika simu yakati za usiku kiasi cha mrembo huyo kutaka kubadili namba ya simu na pia inasemekana picha zilizotumiwa ni za zamani ambazo chaz baba alimpiga ambazo public haikupata nafasi ya kuziona kumbe ilikuwa ni mbinu ya kuuza tu.

No comments:

Post a Comment