Friday, July 29, 2011

LUDA CHRISS AWASILI TANZANIA TAYARI KWA SHOW YA FIESTA 2011 LEADERS CLUB DAR ES SALAAM

.
Mwanamuziki Ludacris akizungumza jioni hii ndani ya Kempinsk hotel na Clouds TV,mara tu alipowasili jiji Dar..Ludacris ameahidi kukamua vilivyo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011,litakalofanyika jumamosi hii ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar
Muwakilishi wa Prime Time Promotions/Clouds Media Group,Balozi Kidamba akimuongoza Mwanamuziki Ludacris pamoja na watu wake kwenye hoteli aliyofikia -Kempinsk jioni ya leo mara baada ya kuwasili jijini Dar tayari kwa kukamua onesho lake moja ndani ya viwanja vya Lidaz Club jijini Dar.


Ludacris akijiweka sawa kwa ajili ya kurekodiwa na Wana Wa Clouds TV jioni ya leo.
 
Muwakilishi kutoka Prime Time Promotions/Clouds Media Group,Balozi Kidamba akiwafafanulia jambo Wageni aliokuja nao Mwanamuziki Ludacris jioni ya leo akitokea nchini Marekani.

 

MWANAMUZIKI mahiri wa miondoko ya Hip Hop,ambaye pia ni muigizaji wa Filamu ajulikanae kwa jina la Christopher Bryian Bridges a.k.a Ludacris akiwasili leo jioni kwenye uwanja wa ndege wa Mwal Jk Nyerere na kupokelewa na Wenyeji wake.Mwanamuziki huyo ambaye ameletwa nchini na Kampuni Bingwa ya Burudani hapa nchini Prime Time Promotions Ltd/Clouds Media Group na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited kupitia kinywaji chake maalum cha Fiesta 2011, Serengeti Primeum Lager



Monday, July 25, 2011

WAIMBA INJILI KUTOKA FAMILIA MOJA MAARUFU KAMA "J SISTERS " KUZINDUA ALBUM YAO MPYA MWISHONI MWA JULY 2011 PALE DIAMOND JUBILEE




KUNDI BORA LA MZIKI WA INJILI TOKA DAR ES SALAAM LIPO TAYARI KWA UZINDUZI BAAAABKUBWA NDANI YA UKUMBI WA DIMOND JUBILII SIKU YA TAR 31 /7/2011

WAIMBAJI HAO TOKA KTK KANISA LA MITO YA BARAKA CHINI YA ASKOFU BRUNO MWAKIBORWA WAMEDAI WANATARAJIA KUONESHA KITU CHA TOFAUTI KTK MZIKI WA INJILI KUTOKANA NA MAZOEZI YA KUTOSHA WALIOJIANDAA NAYOO

KUNDI HILO LINAUNDWA NA KINA DADA WA NNE(4) TOKA FAMILIA YA MZEE MSHAMMA NA MAMA MSHAMA AMBAYE PIA NI MBUNGE WA JIMBO MOJA HUKO BUKOBA

KINA DADA HAO AMBAO BADO WAPO MASOMONI AMBAPO WAWILI KATI YAO WANASOMA NCHINI MAREKANI NA WAWILI WAPO HAPA HAPA.





KWAKWELI TUNA VITU VINGI VIGENI TUTAVIONESHA SIKU YA UZINDUZI WETU HII NI KUTOKANA KUHUDHURIA MATAMASHA MENGI NJE YA NCHI NA KUJIONEA WANAVYOFANYA HIVYO NA SISI TUTAWAONESHA WATANZANIA SIKU HIYO KITU CHA KIPEKEE NA ZAIDI TUNAOMBA MUNGU ILI SIKU HIYO IKAWE YA TOFAUTI KTK MAISHA YA KILA MMOJA ATAKAYE KUJA KTK UZINDUZI WETU. ALISEMA MWANADADA JENIFFER.



Mungu abariki shughuli hii Aamen!!!!!!!!!




Friday, July 22, 2011

KARIUA INVESTMENT YAFANYA KONGAMANO KUBWA KWA WAKALA WA M-PESA WA JIJI LA MWANZA

Kampuni ya Kariua Investment inayojihusisha na usimamizi wa shughuli za mawakala wa kifedha kwa njia ya M-pesa imefanya semina kwa mawakala wake mapema wiki hii, dhumuni la semina hii ni kuwapa mbinu mpya za utendaji kazi na kutambua huduma mpya zinazopatikana katika huduma hiyo ya M pesa, mafunzo hayo yaliyoambatana na hafla ya chakula cha jioni ilifanyika katika hotel ya MIDLAND  iliyopo jijini Mwanza

Umakini unakuwa mkubwa ktk ufuatiliaji wa ajenda moja baada ya nyingine.




Darasa likiendelea



M-blogishaji nami nilikuwa mmoja wa waalikwa wa chakula cha jioni




Jeremiah Mahalu mmoja kati ya wafanyakazi machachari wa kampuni hiyo akifanya utani na moja ya wakala wake

Baadhi ya wakala walioitikia wito na kupokea mbinu za kuwanasa wateja


Dada Eva wa Kariua Inv. na wakala Gahanga ....

Hajji Mhassa kutoka Kariua Inv. akiwa na Elizabeth hakua nyuma....



Trainer wa Wakala wapya wa M pesa  George Mashigila (kulia) akitafakari mambo yaliyozungumzwa katika kongamano



Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Kariua Investment Mwanabure 'Dada Mwana' baada ya kuhitimisha kuwapa madini mapya wakala




 Picha ya pamoja Blogger Tony Sambuka (Kushoto), Sales manager Richard (kati) na Mr. George Mashigila


 Miraj Yussuph kutoka Kariua Inv. akijianda tushusha nyundo zake kwa wakala waliohudhuria kongamano





Wednesday, July 20, 2011

WALIMBWENDE WANAOWANIA U-MISS LAKEZONE 2011 HAWA HAPA...

SHINDANO la kumsaka mrembo wa Kanda ya Ziwa ‘Miss Lake Zone’ linatarajiwa kufanyika Julai 23 ndani ya Meli ya mv Umoja katika Ziwa Victoria.
Mratibu wa shindano hilo, Omari Bakari, alisema warembo 15 kutoka mikoa yote ya ukanda huo wa Ziwa, watakachuana katika shindano hilo leo wanatarajiwa kuingia kambini.
Alisema lengo la kufanya shindano hilo ni katika kuwapa raha mashabiki wa tasnia hiyo ambapo meli hiyo yenye uwezo wa kubeba zaidi ya watu 2,000, siku hiyo itasogezwa kidogo majini kisha kutia nanga na kufanyika kwa zoezi hilo maalumu.
Alisema, tangu Tanzania ipate Uhuru wake mwaka 1961 halijawahi kufanyika shindano la namna hiyo, na kwamba hii ni mara ya kwanza kwa kampuni yao kufanya hivyo.
“Naamini itakuwa ni historia kwani kila mtu atahitaji kuja kushuhudia mchuano huu mkali. Na kila mrembo atahitaji aibuke mshindi dhidi ya wenzake, maandalizi haya yataitangaza vizuri sana Kanda ya Ziwa na taifa kwa ujumla mbele ya ulimwengu wa leo,” alisema.
Kwa upande wa burudani, shindano hilo litapambwa na Maunda Zoro, Hussein Machozi, Isha Mashauzi na kundi la la Obbsecion.
Lydia Mlimi (21) Mara





Jackline Dismas (20) Shinyanga
Sylvia Anatory (19) Kagera
Jaanath Abdul (21) Kagera
Edisa Sixmund (20) Kagera
Monicah James (22) Mwanza
Tracy Sospeter (20) Shinyanga
Joela Lazaro (20) Mwanza
Lilian Rwechungura (21) Geita
Diana Joseph (20) Mwanza
Lydia Fredric (19) Geita
Tausi Ally (21) Geita
Violeth Paschal (18) Mara
Glory Samwel (19) Shinyanga
Irene Karugaba (21) Mwanza
Kakeya Paulo (18) Mara
picha za pamoja walizopiga walimbwende hao mapema wiki hii




Wednesday, July 6, 2011

HABARI PICHA ZA MACHAFUKO YALIYOTOKEA JIJINI MWANZA ASUBUHI YA LEO

uumoja ya mtaa maarufu jijini hapo MAKOROBOI ukiwa umefungwa kuhofia vurugu


Hadi sasa idadi ya watu waliofariki dunia kwa kupigwa risasi imefkia watu watatu
Mungu azilaze roho zao mahala pema peponi - Aamen 
picha kwa hisani ya G-SENGO