Wednesday, July 20, 2011

WALIMBWENDE WANAOWANIA U-MISS LAKEZONE 2011 HAWA HAPA...

SHINDANO la kumsaka mrembo wa Kanda ya Ziwa ‘Miss Lake Zone’ linatarajiwa kufanyika Julai 23 ndani ya Meli ya mv Umoja katika Ziwa Victoria.
Mratibu wa shindano hilo, Omari Bakari, alisema warembo 15 kutoka mikoa yote ya ukanda huo wa Ziwa, watakachuana katika shindano hilo leo wanatarajiwa kuingia kambini.
Alisema lengo la kufanya shindano hilo ni katika kuwapa raha mashabiki wa tasnia hiyo ambapo meli hiyo yenye uwezo wa kubeba zaidi ya watu 2,000, siku hiyo itasogezwa kidogo majini kisha kutia nanga na kufanyika kwa zoezi hilo maalumu.
Alisema, tangu Tanzania ipate Uhuru wake mwaka 1961 halijawahi kufanyika shindano la namna hiyo, na kwamba hii ni mara ya kwanza kwa kampuni yao kufanya hivyo.
“Naamini itakuwa ni historia kwani kila mtu atahitaji kuja kushuhudia mchuano huu mkali. Na kila mrembo atahitaji aibuke mshindi dhidi ya wenzake, maandalizi haya yataitangaza vizuri sana Kanda ya Ziwa na taifa kwa ujumla mbele ya ulimwengu wa leo,” alisema.
Kwa upande wa burudani, shindano hilo litapambwa na Maunda Zoro, Hussein Machozi, Isha Mashauzi na kundi la la Obbsecion.
Lydia Mlimi (21) Mara





Jackline Dismas (20) Shinyanga
Sylvia Anatory (19) Kagera
Jaanath Abdul (21) Kagera
Edisa Sixmund (20) Kagera
Monicah James (22) Mwanza
Tracy Sospeter (20) Shinyanga
Joela Lazaro (20) Mwanza
Lilian Rwechungura (21) Geita
Diana Joseph (20) Mwanza
Lydia Fredric (19) Geita
Tausi Ally (21) Geita
Violeth Paschal (18) Mara
Glory Samwel (19) Shinyanga
Irene Karugaba (21) Mwanza
Kakeya Paulo (18) Mara
picha za pamoja walizopiga walimbwende hao mapema wiki hii




No comments:

Post a Comment