Wednesday, May 25, 2011

EXCLUSIVE: HURUMA ZIMEMPONZA MH.WILLIAM LUKUVI..!!


Waziri William lukuvi ameibuka na kujibu tuhuma za ufisadi wa kujimilikisha vitalu dhidi yake kwa kudai alipewa kibali toka mamlaka husika na baada ya kuvuna mbao alizigawa.
 Awali maombi ya mbao hizo ilikuwa kaomba msaada wa kuikarabatia shule yake iliyopatwa na janga la kuteketezwa kwa moto ili ikarabatiwe upya shule hiyo lakini kutokana na huruma za waziri huyo alizigawa mbao hizo kwa watu binafsi.
"unajua mimi nina huruma sana hata ukinipa nifanye biashara ya karanga ntazigawa zote" alisema lukuvi,hata hivyo bado tunasubiri Dk.Slaa ajibu maoni ya Mh.lukuvi kuwa Dk.Slaa ni mtu wa porojo tu.

ILIVOKUA JIJINI MWANZA

ROCK CITY SARS na wageni  wao Bongo Movie mazoezini kabla ya match

Friday, May 20, 2011

VIKOSI VYA BONGO MOVIE v/s DJs VITACHOCHEZA JUMAPILI HII JIJINI MWANZA HIVI HAPA

Kikosi kizima kitakachotua jijini Mwanza siku ya Jumamosi kimetajwa rasmi tayari kwa ziara hiyo.Kikosi hicho ambacho kitatua jijini Mwanza tayari kwa mchezo wao utakaowakutanisha na Watangazaji na Madj wa wa mji huo kinajumuisha wanaume na wanawake.Kikosi hicho ni kama ifuatavyo:

Hartman,Jacob Stephen (JB),Chiki Mchoma, Rado, Richie Richie,  Ray,  Cloud,Kiduku,   Jimmy Master,  Salehe,  Steven Nyerere,  Bitebo,     Masanja Mkandamizaji ,  Kupa,  Jimmy Mafufu,   Ben Kinyaiya,    Tinno,   Taff,  Malima, Shija. Wanawake watakaongozana na 

Timu ni Wema Sepetu, Mainda,Jackline Wolper,  Odama, Jackline Pentezel, Maya, Snura


MA DJs na watangazaji HAWA HAPA!!!!


Timu ya Madj na Watangazaji inaundwa na Dj John,Dj Chriss,  Dj Maliz,  Dj Cutter,Ally Coco,Fred wa kaka bonda,  Filbert kabago,  Muhsin Mambo.   Dj Simba,  Jeff Jerry na Uncle Sam na wengine wengi tuu.  Burudani itakuwa kubwa siku hiyo kwani Bongo Movie Fc wanakuja kamili kamili.  Mastar wote wa Filamu siku hiyo watakuwa ndani ya CCM Kirumba kutoa burudani ya kutosha kwa mashabiki watakaofika.

BREAKING NYUZZZZZZ, SHEIKH YAHAYA AFARIKI DUNIA

WEMA SEPETU MCHARUKO WAMPANDA AMSUTA CHAZ BABA


Chaz baba akipata mafundo ya mate toka kwa wema enzi za uhai wa penzi lao
      Mrembo alietumia nafasi ya sanaa vibaya Wema sepetu amefunguka dhidi ya tuhuma zilizotapakaa kila kona ya nchi kuwa karudiana na Chaz baba na kuwa hamtaki tena Diamond kwakua hayawezi mabo ya kitandani.

                 Wema alisema kuwa bado anampenda sana Diamond na hana hisia zozote za kuachana na kijana huyo msharobalo alietingwa na mawazo ya kuachwa muda wowote kwani ndege usipomshika vizuri hukuachia manyoya ndiyo hali aliyonayo diamond kwa sasa.
                 "Chaz baba nilishamwaga na nilishamwambia kuwa siwezi kuwa nawe tena ila anatumia magazeti kuandika habari za uongo kwani mimi ndiye niliempa umashuhuri mpaka akawa anaandikwa mara kwa mara sasa ameona haandikwi kama zamani ndiyo maana ameamua kutafuta ujiko kupitia mimi" wema alitonya haya kwa kimombo.
                  Inasemekana Chaz baba amekuwa akimsumbua wema katika simu yakati za usiku kiasi cha mrembo huyo kutaka kubadili namba ya simu na pia inasemekana picha zilizotumiwa ni za zamani ambazo chaz baba alimpiga ambazo public haikupata nafasi ya kuziona kumbe ilikuwa ni mbinu ya kuuza tu.

Thursday, May 19, 2011

AMBER ROSE NA MAUZO YA FRONT PAGE

Amber rose amepata shavu la kuuza front page katika jarida la king kwa mara nyingine.

Monday, May 16, 2011

DJ DAVY MTAMBONI CLUB LIPS MWANZA!!!!!

Usiache kuwepo pale @club_lips ya Isamilo Lodge weekend hii na kila weekend, 
mtu mzima Dj Davy anakuepo kwenye 1 na 2 kwa yako buku tano tu. 
Njoo ujionee club mpya na yakisasa /yakijanja kanda ya ziwa