Thursday, October 25, 2012

Baadhi ya warembo watakao shiriki kinyang'anyiro cha miss Ilemela kinachotarajiwa kufanyika tarehe 26/05/2012 kwa mara ya kwanza katika ukumbi mkubwa wa GOLD CREST HOTEL jijini Mwanza.

Wednesday, May 30, 2012



TAREHE YA MISS NYAMAGANA  KUFANYIKA IJUMAA YA JUNE 01, 2012
Warembo 20 kutoka wilaya ya Nyamagana Mwanza.
Stoppers Entertainment inakuletea Miss Nyamagana 2012 Mwanza. Warembo wenye Haiba, Tabasamu, Minato na Catwalk ya uhakika.
Shindano litafanyika ijumaa ya tarehe 01 june 2012, saa 2 usiku katika ukumbi wa Nyerere uliopo katika hoteli ya Gold crest Mwanza.
Kwa kiingilio cha Tsh 20,000/- Mashabiki watashuhudia shindano hilo.
Burudani ni pamoja Mwanamuziki Linah, mara baada ya ziara yake ya nchini Marekani, show yake ya kwanza, itakua jijini Mwanza, Mwingine ni Ditto kutoka THT, pamoja na mwanamuziki Hafsa Kazinja aliyetamba na kibao chake cha Pressure akimshirikisha Banana Zorro.
MC au Mshehereshaji mkuu katika shindano hilo ni muigizaji maarufu katika tasnia ya uchekeshaji namzungumzia Mpoki.

Wednesday, August 3, 2011

BREAKING NEWZ: RAMSEY NOAH ADONDOKA GHOROFANI


-->

Ramsey Noah amenusurika kifo baada ya kuanguka toka ghorofani wakati ana shoot movie mpya akiwa nchini Ghana.
Ramsey alikua on set na actors Nana Ama McBrown,Beverly Afaglo,Roslyn Ngissah,Nana Hayford wakiwa wnajiandaa Hotel Babylon,Where Clothes Are Naked chini ya directer Kobi Rana,Na alianguka toka kwenye ghorofa na inasemekana Ramsey ameumia kwa ndani kitaalamu wanaita internal bleeding baada ya kulalamika maumivu ya tumbo huku akitoka damu mdomoni na kupewa huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa hospitali jijini Accra.Ramsey alishawahi kupata ajali ya pikipiki mwaka 2007 na ajali hiyo na ameweka jino la bandia.

Monday, August 1, 2011

INTER ZEPHA TANZANIA LIMITED JIJINI MWANZA YATOA ZAWADI KWA MSHINDI.


Afisa mauzo na masoko wa Inter zepha Tanzania Limited Mr.Hamisi S. Fupi akitoa zawadi kwa mshindi.

Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Pamba Sekondari ya jijini Mwanza walioshuhudia tukio hilo.

Washindi walioshinda katika Essay writing competition, kutoka kulia ni Renatus Hemed (head prefect) mshindi wa 3 ,Mayala P Mapinda mshindi wa 1 na Samwel J Mtiba mshindi wa 2.

Wanafunzi wakijumuika katika picha ya pamoja kumpongenza mshindi Mayala P Mapinda.

Inter zepha Tanzania Limited ya jijini la Mwanza imetoa zawadi kwa mshindi wa shindano la essay writing competition lililofanyika katika shule ya sekondari pamba ya jijini mwanza. Shindalo hilo lililo jumuisha wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 baada ya kampuni kufanya Semina kuhusu ICT Aweaness iliyofanyika tar 15 july na kutoa zoezi la kuandika essay juu ya umuhimu wa tekinolojiya ya habari na mawasiliano katika elimu ambapo kampuni hiyoilitoa ahadi kutoa zawadi ya lap top kwa mshindi.

Interzepha inatoa pongezi kwa Mayala P mapinda wa kidato ya 5 CBG kwa kuwa mshindi la shindalo hilo.pia tunatoa shukurani za dhat kwa wanafunzi wote walioshiriki.

Friday, July 29, 2011

LUDA CHRISS AWASILI TANZANIA TAYARI KWA SHOW YA FIESTA 2011 LEADERS CLUB DAR ES SALAAM

.
Mwanamuziki Ludacris akizungumza jioni hii ndani ya Kempinsk hotel na Clouds TV,mara tu alipowasili jiji Dar..Ludacris ameahidi kukamua vilivyo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011,litakalofanyika jumamosi hii ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar
Muwakilishi wa Prime Time Promotions/Clouds Media Group,Balozi Kidamba akimuongoza Mwanamuziki Ludacris pamoja na watu wake kwenye hoteli aliyofikia -Kempinsk jioni ya leo mara baada ya kuwasili jijini Dar tayari kwa kukamua onesho lake moja ndani ya viwanja vya Lidaz Club jijini Dar.


Ludacris akijiweka sawa kwa ajili ya kurekodiwa na Wana Wa Clouds TV jioni ya leo.
 
Muwakilishi kutoka Prime Time Promotions/Clouds Media Group,Balozi Kidamba akiwafafanulia jambo Wageni aliokuja nao Mwanamuziki Ludacris jioni ya leo akitokea nchini Marekani.

 

MWANAMUZIKI mahiri wa miondoko ya Hip Hop,ambaye pia ni muigizaji wa Filamu ajulikanae kwa jina la Christopher Bryian Bridges a.k.a Ludacris akiwasili leo jioni kwenye uwanja wa ndege wa Mwal Jk Nyerere na kupokelewa na Wenyeji wake.Mwanamuziki huyo ambaye ameletwa nchini na Kampuni Bingwa ya Burudani hapa nchini Prime Time Promotions Ltd/Clouds Media Group na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited kupitia kinywaji chake maalum cha Fiesta 2011, Serengeti Primeum Lager



Monday, July 25, 2011

WAIMBA INJILI KUTOKA FAMILIA MOJA MAARUFU KAMA "J SISTERS " KUZINDUA ALBUM YAO MPYA MWISHONI MWA JULY 2011 PALE DIAMOND JUBILEE




KUNDI BORA LA MZIKI WA INJILI TOKA DAR ES SALAAM LIPO TAYARI KWA UZINDUZI BAAAABKUBWA NDANI YA UKUMBI WA DIMOND JUBILII SIKU YA TAR 31 /7/2011

WAIMBAJI HAO TOKA KTK KANISA LA MITO YA BARAKA CHINI YA ASKOFU BRUNO MWAKIBORWA WAMEDAI WANATARAJIA KUONESHA KITU CHA TOFAUTI KTK MZIKI WA INJILI KUTOKANA NA MAZOEZI YA KUTOSHA WALIOJIANDAA NAYOO

KUNDI HILO LINAUNDWA NA KINA DADA WA NNE(4) TOKA FAMILIA YA MZEE MSHAMMA NA MAMA MSHAMA AMBAYE PIA NI MBUNGE WA JIMBO MOJA HUKO BUKOBA

KINA DADA HAO AMBAO BADO WAPO MASOMONI AMBAPO WAWILI KATI YAO WANASOMA NCHINI MAREKANI NA WAWILI WAPO HAPA HAPA.





KWAKWELI TUNA VITU VINGI VIGENI TUTAVIONESHA SIKU YA UZINDUZI WETU HII NI KUTOKANA KUHUDHURIA MATAMASHA MENGI NJE YA NCHI NA KUJIONEA WANAVYOFANYA HIVYO NA SISI TUTAWAONESHA WATANZANIA SIKU HIYO KITU CHA KIPEKEE NA ZAIDI TUNAOMBA MUNGU ILI SIKU HIYO IKAWE YA TOFAUTI KTK MAISHA YA KILA MMOJA ATAKAYE KUJA KTK UZINDUZI WETU. ALISEMA MWANADADA JENIFFER.



Mungu abariki shughuli hii Aamen!!!!!!!!!




Friday, July 22, 2011

KARIUA INVESTMENT YAFANYA KONGAMANO KUBWA KWA WAKALA WA M-PESA WA JIJI LA MWANZA

Kampuni ya Kariua Investment inayojihusisha na usimamizi wa shughuli za mawakala wa kifedha kwa njia ya M-pesa imefanya semina kwa mawakala wake mapema wiki hii, dhumuni la semina hii ni kuwapa mbinu mpya za utendaji kazi na kutambua huduma mpya zinazopatikana katika huduma hiyo ya M pesa, mafunzo hayo yaliyoambatana na hafla ya chakula cha jioni ilifanyika katika hotel ya MIDLAND  iliyopo jijini Mwanza

Umakini unakuwa mkubwa ktk ufuatiliaji wa ajenda moja baada ya nyingine.




Darasa likiendelea



M-blogishaji nami nilikuwa mmoja wa waalikwa wa chakula cha jioni




Jeremiah Mahalu mmoja kati ya wafanyakazi machachari wa kampuni hiyo akifanya utani na moja ya wakala wake

Baadhi ya wakala walioitikia wito na kupokea mbinu za kuwanasa wateja


Dada Eva wa Kariua Inv. na wakala Gahanga ....

Hajji Mhassa kutoka Kariua Inv. akiwa na Elizabeth hakua nyuma....



Trainer wa Wakala wapya wa M pesa  George Mashigila (kulia) akitafakari mambo yaliyozungumzwa katika kongamano



Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Kariua Investment Mwanabure 'Dada Mwana' baada ya kuhitimisha kuwapa madini mapya wakala




 Picha ya pamoja Blogger Tony Sambuka (Kushoto), Sales manager Richard (kati) na Mr. George Mashigila


 Miraj Yussuph kutoka Kariua Inv. akijianda tushusha nyundo zake kwa wakala waliohudhuria kongamano





Wednesday, July 20, 2011

WALIMBWENDE WANAOWANIA U-MISS LAKEZONE 2011 HAWA HAPA...

SHINDANO la kumsaka mrembo wa Kanda ya Ziwa ‘Miss Lake Zone’ linatarajiwa kufanyika Julai 23 ndani ya Meli ya mv Umoja katika Ziwa Victoria.
Mratibu wa shindano hilo, Omari Bakari, alisema warembo 15 kutoka mikoa yote ya ukanda huo wa Ziwa, watakachuana katika shindano hilo leo wanatarajiwa kuingia kambini.
Alisema lengo la kufanya shindano hilo ni katika kuwapa raha mashabiki wa tasnia hiyo ambapo meli hiyo yenye uwezo wa kubeba zaidi ya watu 2,000, siku hiyo itasogezwa kidogo majini kisha kutia nanga na kufanyika kwa zoezi hilo maalumu.
Alisema, tangu Tanzania ipate Uhuru wake mwaka 1961 halijawahi kufanyika shindano la namna hiyo, na kwamba hii ni mara ya kwanza kwa kampuni yao kufanya hivyo.
“Naamini itakuwa ni historia kwani kila mtu atahitaji kuja kushuhudia mchuano huu mkali. Na kila mrembo atahitaji aibuke mshindi dhidi ya wenzake, maandalizi haya yataitangaza vizuri sana Kanda ya Ziwa na taifa kwa ujumla mbele ya ulimwengu wa leo,” alisema.
Kwa upande wa burudani, shindano hilo litapambwa na Maunda Zoro, Hussein Machozi, Isha Mashauzi na kundi la la Obbsecion.
Lydia Mlimi (21) Mara





Jackline Dismas (20) Shinyanga
Sylvia Anatory (19) Kagera
Jaanath Abdul (21) Kagera
Edisa Sixmund (20) Kagera
Monicah James (22) Mwanza
Tracy Sospeter (20) Shinyanga
Joela Lazaro (20) Mwanza
Lilian Rwechungura (21) Geita
Diana Joseph (20) Mwanza
Lydia Fredric (19) Geita
Tausi Ally (21) Geita
Violeth Paschal (18) Mara
Glory Samwel (19) Shinyanga
Irene Karugaba (21) Mwanza
Kakeya Paulo (18) Mara
picha za pamoja walizopiga walimbwende hao mapema wiki hii